Bolt kuuaga ulimwengu wa riadha - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 1 August 2017

Bolt kuuaga ulimwengu wa riadha


https://edusportstz.blogspot.com/
Anafahamika kwa kutimka kwa kasi ya radi! Usain Bolt ambaye anajiandaa kushiriki mashindano yake ya mwisho kabisa ya ubingwa wa Dunia yatakayoandaliwa jijini London kuanzia Agosti nne hadi 13.


Mahasimu wa Bolt watakuwa, kwa mara ya kwanza, na furaha kumwona akiondoka mtu ambaye ametawala mbio za masafa mafupi duniani kwa mwongo mmoja uliopita, lakini mchezo wa riadha hautakuwa na shauku kuhusu kumpa kwaheri ya mwisho Mjamaica huyo.

Bolt alitawala katika michezo mitatu ya mwisho ya Olimpiki na kama hangeondolewa kabla ya fainali ya mita 100 mjini Daegu mwaka wa 2011, mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 30 angeweza kutawala michezo minne ya mwisho ya Olimpiki.


Gatlin anasema ilikuwa heshima kushindana na Bolt

Sasa swali ni je, nani ataweza kuchukua nafasi yake juu ya jukwaa la mbio za mita 100? Bingwa wa zamani wa Olimpiki na dunia Justion Gatlin, anatoa maoni yake "Yatakuwa mashindano ya kufurahisha zaidi kwa sababu ni wakati maalum sio kwangu tu na Usain Bolt lakini kuna wanariadha wengine wengi vijana ambao wanachipuka. Nadhani hicho ndio kitakachokuwa maalum kuhusu sio tu nani atakayeweza kujaza pengo katika mchezo wetu lakini litajazwa na wanariadha vijana ambao wapo kwa sasa na wanataka kujitengenezea jina hivyo utakuwa wakati wa kusisimua na wa mabadiliko kwa wengi".

Na je, Gatlin anasemaje kuhusu kuwa na fursa ya mwisho kumpiku Usain Bolt katika mashindano ya London? "sitoshiriki na mawazo hayo. sitoshiriki kwa ajili ya kujifurahisha tu. Najaribu hasa kuweka pamoja Justin wawili ambapo nataka tu kushiriki kwa kufurahia kama tu iliyvokuwa chuoni na bado niweze kutawala lakini pia nataka kushiriki kwa kuangazia wakati maalum ambao ni wa mabadiliko ya kihistoria. Hivyo utaona kiasi mambo hayo yote mawili. Ntakwenda tu kuwa na wakati mzuri.

Bolt atastaafu baada ya mashindano ya London na hivyo kuwapa nafasi wanariadha wengine chipukizi kujaribu kuvaa viatu vyake. Lakini kama mwanariadha yeyote anaweza kukaribia kuifikia rekodi ya Bolt na haiba yake ni suala jingine tofauti.