​​​​​​​Beki wa Chapecoense arejea tena uwanjani - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 1 August 2017

​​​​​​​Beki wa Chapecoense arejea tena uwanjani
Beki Alan Ruschel, aliyenusurika ajali ya ndege mwaka jana ambayo iliwaua wenzake 19 wa timu ya Chapecoense, anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza kabisa wakati timu yake itashuka dimbani dhidi ya miamba Barcelona
Ruschel alikuwa miongoni mwa manusura sita wakati ndege hiyo, iliyokuwa imewabeba watu 77, ilianguka katika eneo la milima nchini Colombia kabla ya mchuano wao wa mkondo wa kwanza wa fainali ya dimba la Copa Sudamericana dhidi ya Atletico Nacional Medellin mnamo Novemba 22.

Alifanyiwa upasuaji kwenye mgongo wake na sasa amerejea mazoezini na atacheza uwanjani Camp Nou dhidi ya Barca katika mtanange wa kirafiki mnamo Agosti saba. Taarifa ya tovuti ya klabu ya Chapecoense imesema kurejea kwa Ruschel ni hatua muhimu kwake kupona kikamilifu na pia mchakato wa kukijenga upya kikosi chao. Ruschel alinusurika ajali hiyo pamoja na beki Neto na mlinda lango Jakson Follmann, aliyekatwa sehemu ya mguu wake.