Rooney asepa na Wachezaji wanne wa Bongo - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 15 July 2017

Rooney asepa na Wachezaji wanne wa Bongo
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba amesema wanatarajia kuandaa mpango maalumu wa kuwasaidia wachezaji wa hapa nchini angalau wanne kila mwaka kwenda England kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.

“Tunataka soka la Tanzania ilipige hatua ili siku moja na sisi tuwe na wachezaji wanaocheza katika Ligi Kuu England.


“Tunajipanga ili tuweze kuleta maskauti hapa nchini kwa ajili ya kuangalia wachezaji na ikiwezekana angalau kila mwaka Watanzania wanne waweze kwenda England kwa ajili kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa ili siku moja tuweze kuwaona wakipambana na akina Rooney katika ligi kuu ya nchi hiyo,” alisema Tarimba.

No comments:

Post a Comment