MSUVA: ASANTENI SANA YANGA - EDUSPORTSTZ

Latest

MSUVA: ASANTENI SANA YANGA



Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva.

NDOTO ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva ya kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi ilitimia juzi Jumatano baada ya kiungo huyo kupaa hadi nchini Morocco kwa ajili ya kumalizana na DifaĆ¢ Hassani El Jadidi kabla ya kujiunga nayo rasmi.

Msuva anaikacha Yanga aliyodumu nayo kwa miaka mitano tangu alipoh a mia klabuni hapo akitokea Moro United mwaka 2012, baada y a kukamilika kwa dili hilo ambalo limesimamiwa na meneja wake, Jonas Tiboroha. Ndani ya klabu hiyo ya Difaa El Jadidi, Msuva ataungana na winga, Ramadhan Singano ‘Messi’ ambaye alishatangulia kujiunga na kikosi hicho akitokea Azam FC ambayo alimaliza mkataba.



Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa saba wa Kitanzania kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi. Wengine ni Rashid Mandawa aliyepo Botswana, Elias Maguri anayecheza Oman, Thomas Ulimwengu (Sweden), Mbwana Samatta (Ubelgiji), Farid Mussa (Hispania) na Abdi Banda aliyejiunga na Baroka FC ya Afrika Kusini. M u d a mfupi kabla ya Msuva kukwea pipa kuelekea Morocco juzi Jumatano, Championi Ijumaa, lilipata nafasi ya kuzungumza naye na hapa anafunguka kama ifuatavyo:


Simon Msuva.

NINI UTAKACHOKIKUMBUKA NDANI YA YANGA?

“Daaah! Kuna vitu vingi sana nitavimisi baada ya kuondoka Yanga, siwezi kuvielezea sana lakini kikubwa ni juu ya utani ambao niliuzoea kutoka kwa wachezaji wenzangu, lakini hata kuzurura kwani nilishazoea nikitokea mazoezini naenda maskani ila huko Morocco sidhani kama nitafanya hivyo. “Nikiwa huko nitawakumbuka sana washikaji zangu ambao wamenifanya niwe hapa na wale ambao nimekaa na kushirikiana nao kwa kipindi chote nikiwa Yanga.



UMEJIPANGAJE KUISHI NJE YA TANZANIA?

“Sehemu yoyote ile ukishazoea basi hakuna tatizo lolote lile, najua nitakuwa mgeni kwa siku kadhaa zile za mwanzo lakini baada ya hapo mambo yataenda vizuri. “Itakuwa siyo rahisi kwani huko kila kitu ni kipya ila nitazoea na kuendana na maisha ya huko, kikubwa ni suala la muda tu na kujichanganya na wenzangu.

VIPI KUHUSU LUGHA YAO, INAPANDA? “Sijajua maana nitakuta wanazungumza lugha gani lakini ukija kwenye soka haitakuwa ngumu kuwasiliana na wenzangu kwani mnapokuwa uwanjani mnaongea lugha moja tu ya kimpira. “Shida itakuwa kwenye vitu vingine jinsi ya kuvipata ila uwanjani sitapata sana taabu, lakini kadiri nitakavyokaa ndivyo nitazoea tu sina hofu na hilo.



UNAIONAJE YANGA YA SASA?

“Iko vizuri, hakuna tofauti na timu am
bayo mimi naiacha na ile ya msimu uliopita kwani wachezaji wengi wamebaki na hata kwa wale waliondoka nafasi zao zimezibwa vizuri. “Ukinitoa mimi ninayeondoka naamini hawa waliobaki wataifanya kazi nzuri na kuendeleza mafanikio ambayo tumeyapata wakati ambao nilikuwepo.

UNAJISIKIAJE UNAVYOIACHA YANGA?

“Kiukweli natamani niendelee kuwepo lakini ndiyo hivyo hakuna namna, umeshafika wakati sasa inabidi niondoke kwenda kucheza soka sehemu nyingine tofauti na Yanga. “Najisikia vibaya kuachana na sehemu niliyopata furaha, lakini hakuna namna inanibidi tu niondoke nikatafute maisha sehemu nyingine.

NINI MIPANGO HUKO?

“Nimejipanga kucheza kwa muda mfupi na kwa juhudi kubwa ili nionekane na timu nyingine, sitaki safari yangu iishie Morocco, namaani s h a k w a m b a nitaondoka huko kama nilivyofanya hapa Yanga. “Hiyo ni njia tu ya kwenda kucheza soka Ulaya, kama a m b a v y o n i m e k u w a nikiwaza nifike alipo m s h a m b u l i a j i mwenzangu, Mbwana Samatta ambaye kila mara amekuwa akinipa moyo wa kupambana. Unadhani itakuwa rahisi kutamba Morocco? “Hakuna linaloshindana, naamini kama nikicheza kwa juhudi kubwa na kufuata maelekezo ya kocha atakayonipa basi nina nafasi kubwa ya kuendeleza kile ambacho nimekifanya kwa miaka mitano niliyokaa hapa Yanga,” anasema Msuva.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz