MOURINHO: SINA MPANGO NA BALE KWA SASA - EDUSPORTSTZ

Latest

MOURINHO: SINA MPANGO NA BALE KWA SASA





Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho.

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amese­ma hana mpan­go wa kumsa­jili mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale, kwenye kipindi hiki cha usajili.

Bale amekuwa akitajwa mara kwa mara kuwa anawe­za kujiunga na Manchester United aki­tokea Real Madrid, la­kini Mour­inho am­baye ame­wa hikumfundisha kiungo huyo mshambuliaji amesema hana mpan­go naye kwa sasa.

Mourinho amesema kwa sasa Bale ana fu­raha kwenye kikosi cha Madrid na litakuwa jambo gumu kwake kuondoka kwenye timu hiyo ya Hispania.

Mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale.

Hata hivyo, im­eelezwa kuwa Unit­ed wanaendelea kumwania winga wa Inter Milan, Ivan Perisic, kwa kitita cha pauni mil­ioni 48, zaidi ya shilingi bilioni 136.

United wamekuwa wakitakiwa kutoa kitita cha pauni milioni 100, kama wanamtaka Bale jambo ambalo limekuwa gumu sana kwa United kwa sasa.

Madrid wa­naweza kuwa na wazo la ku­muuza staa huyo kama tu watafanikiwa k u m p a t a staa wa Mo­naco, Kylian Mbappe.

“Sijawahi k u f i k i r i kuhus u B a l e k u o n ­doka Ma­drid kwa sasa, nao­n a kuwa ana fu­raha na anataka kubaki kwenye timu hiyo.

“Ni rahisi kufahamu mchezaji ambaye anawe­za kusajiliwa kwa sasa, lakini siyo Bale, kwa kuwa bado anataka kubaki kwenye timu hiyo.

“Yupo kwenye timu ambayo ina maslahi ma­zuri na inafanya vizuri uwanjani siyo jambo ra­hisi kuondoka hapo,” al­isema Mourinho kocha wa zamani wa Real Ma­drid, Porto, Inter Milan na Chelsea.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz