BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 25 July 2017

MASTAA WA SIMBA WALIOKUWA RWANDA KUTIMKIA SAUZI LEO
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara.

Wachezaji wa kikosi cha Simba waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Starswanatarajiwa kuondoka leo jijini Dar es Salaam kwenda Johannesburg nchini Afrika Kusini ili kujiunga na wenzao waliopo nchini humo kwa ajili ya kambi.

Kikosi cha Simba kipo Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya kambi kuelekea msimu ujao wa 2017/18. Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema wachezaji hao wanaweza kumjumuisha kipa Aishi Manula ambaye bado usajili wake inadaiwa kuwa haujakamilika, wengine ni Said Mohammed, Shomari Kapombe, Salim Mbonde, Erasto Nyoni, Muzamiru Yassin, Shiza Kichuya, Said Ndemla na John Bocco.Taifa Stars iliondolewa katika mbio za kuwania kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN), baada ya kulazimishwa 0-0 na Rwanda jijini Kigali.

Matokeo hayo yanamaanisha Taifa Stars inaondolewa kwa bao la ugenini, kufuatia kulazimishwa sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza Jumamosi ya wiki iliyotangulia.

No comments:

Post a Comment