;
Himidi Mao afunguka kirusi kilichotafuna ushindi wa Stars dhidi Rwanda jana - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 16 July 2017

Himidi Mao afunguka kirusi kilichotafuna ushindi wa Stars dhidi Rwanda janaNahodha wa Taifa Stars, Himid Mao amefunguka sababu kubwa iliyopelekea Stars kushindwa kupata matokeo mazuri katika mchezo wa jana dhidi ya Rwanda katika mchezo wa kwanza kusaka kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan 2018).

Himid Mao ambaye aliweza kuisawazishia Taifa Stars goli kwa njia ya penati katika dakika 34 amesema mchezo huo kwa Stars ulikuwa mgumu kutokana na kuruhusu goli la mapema kutoka kwa Rwanda jambo ambalo lilipelekea kuharibu mpangilio wa mechi hiyo.

"Ugumu ni kama ambavyo nimesema tuliruhusu goli la mapema kutoka kwa wapinzani wetu kwa hiyo hata 'game plan' yetu ilibidi ibadilike kuanzia hapo ili tuweze kusawazisha na kuongeza wakati kama tungekuwa hatujafungwa goli moja lingeweza kutupa ushindi wa mchezo" alisema Himid Mao

Mbali na hilo Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga naye alifunguka na kusema kuwa kwa matokeo hayo ya sare ambayo si mazuri kwa Taifa Stars hivyo amesema ni jukumu lake yeye pamoja na wenzake kuangalia makosa mbalimbali yaliyojitokeza katika mchezo huo na kuyafanyia marekebisho ili kufanya vizuri zaidi katika mchezo unaofuata.

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB