BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 19 July 2017

Ajibu apewa onyo kaliMshambuliaji mpya wa Yanga, Ibrahim Ajibu.
KOCHA wa Yanga, George Lwandamina, raia wa Zambia, amewapiga ‘biti’ wachezaji wake wote akiwemo mshambuliaji mpya, Ibrahim Ajibu aliyetoka Simba kuhakikisha wanajituma kwenye mazoezi, na ili mchezaji apate namba ndani ya kikosi chake cha kwanza, hataangalia jina badala yake kujituma.

Lwandamina aliyeipa Yanga ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, kwa sasa anakiandaa kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao ambapo wanaendelea na mazoezi yao mara mbili kwa siku, asubuhi gym na jioni uwanjani.

Mzambia huyo ameliambia Championi Jumatano kuwa, hatashindwa kumpiga benchi mchezaji yeyote atakayeshindwa kufanya vizuri kwenye mazoezi ya kikosi hicho.

“Kwenye kikosi cha kwanza cha timu yangu sitaangalia nani mchezaji mkubwa na yupi ni mdogo, badala yake uwezo wa mchezaji binafsi kwenye mazoezi ndiyo ambao utamuwezesha kucheza, na yule ambaye atashindwa kufanya vyema basi sitakuwa na nafasi naye.

“Sitajali hata kama iwe usajili wa karibuni kama ilivyo kwa Ajibu kukaa benchi endapo atazembea mazoezini, nimwambie tu kuwa lazima ajitume mazoezini tena kwa nguvu kubwa na kama siyo hivyo basi atakaa benchi,” alisema kocha huyo.

No comments:

Post a Comment