EDUSPORTSTZ

Edusportstz ni blog maalumu kwa habari za michezo,tetesi za usajili, ligi kuu vpl, epl na laliga pamoja na habri za soka za kimataifa.

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 5 June 2017

WENGER APEWA PAUNI MILIONI 165 ZA USAJILI..AAMBIWA MSIMU UJAO UBINGWA UTUE EMIRATES STADIUM

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye anafahamika kwa ubahili, amepewa kitita kikubwa cha fedha akiambiwa azitumie kufanya usajili wa wachezaji wapya.


Mabosi wa klabu hiyo wamemtengea kocha huyo Mfaransa Pauni 165 milioni na kumweleza azitumie kuimarisha kikosi chake.


Bodi ya klabu hiyo imempa kitita hicho kikubwa cha fedha ili kumwezesha kushindana na wababe wengine England kwenye soko la usajili.


Tayari, Wenger anayo majina ya Riyad Mahrez wa Leicester City na Mturuki Arda Turan ambaye ameachwa na Barcelona.


Wenger ameambiwa awe makini na kikosi chake Arsenal msimu ujao kwani mwisho wa msimu atatakiwa kutwaa taji ambalo amelikosa tangu msimu wa 2004.

No comments:

Post a Comment