Picha ya Beckham na mtoto wake Serengeti imeleta mjadala hadi kwao - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 3 June 2017

Picha ya Beckham na mtoto wake Serengeti imeleta mjadala hadi kwao

Jina la staa wa soka wa zamani wa kimataifa wa England David Beckham limezidi kuchukua headlines baada ya wiki hii kuonekana akiwa Tanzania katika hifadhi ya Serengeti akiwa pamoja na familia yake watoto wake wanne na mkewe Victoria.

Beckham akimbusu mwanae wa mwisho Harper Seven mwenye umri wa miaka mitano wakiwa Serengeti.

Ilijulikana kuwa Beckham yupo Tanzania baada ya kusambaa kwa video fupi akionekana Beckham na familia yake Airport Dar es Salaam, Beckham amepiga picha kadhaa na kuzipost instagram akiwa Serengeti lakini picha na mtoto wake wa mwisho Harper imekuwa topic.Picha aliyopiga David Beckham akimkiss mtoto wake Harper Seven katika lips baadhi ya mashabiki wanaomfollow wameonekana kuikosoa na kuona haipo katika maadili na wengine wakiona haina shida, mjadala ambao umeendelea hadi mtandao wa mirror.co.uk wa England ambapo ndio kwao na David Beckham kuandika mawazo ya mashabiki hao.


Hii sio Tanzania sema hapa yupo pamoja na watoto wake wote wanne Harper, Romeo, Cruz na mtoto wake mkubwa Brooklynbeckham

Baadhi ya comment za mashabiki

“Kwa nini anafanya hivi hatuhitaji kuona”>>>comment ya shabiki

“Wapuuzie wenye mawazo finyu mwanangu ana umri wa miaka 10 na bado na mbusu ni watu wenye matatizo wanaoona hivyo ni vibaya” >>>john_st1234

“Nina miaka 32 na bado nawabusu wazazi wangu wote katika lips nawapenda siku zote na nimekuwa nikiwabusu hata watoto wangu wakiume wote katika lips wana umri wa miaka 6,5 na 2”>>>jul1271

“Kiukweli kumbusu binti yako katika lips kidogo hiyo sio sawa” >>>comment ya shabiki

No comments:

Post a Comment