NEWS ALERT: SHABIKI WA YANGA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Tuesday, 20 June 2017

NEWS ALERT: SHABIKI WA YANGA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI


Globu ya Jamii imepokea taarifa ya kifo cha shabiki maarufu wa timu ya Yanga Ally Mohamed almaarufu kwa jina la Ally Yanga. Taarifa zinaeleza kuwa Ally Yanga amefariki Dunia mapema leo katika ajali ya gari eneo la kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma. Taarifa rasmi tutawaletea kutoka Jeshi la Polisi kutoka mkoani humo. Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-Amin.

Taarifa zinasema Ally Yanga alikuwa kwenye msafara wa mbio za Mwenge kabla ya kupata ajali hiyo barabara ya Wiyenzele kuelekea Chipogoro na kufariki hapo hapo.

Ally aliyezaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya watoto sita, kabla ya umauti wake inafahamika alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam.


Lakini tangu baada ya uchaguzi Mkuu Novemba 2015, Ally Yanga ameadimika viwanja vya soka kutokana na kujikita zaidi kwenye shughuli za Chama cha Mapinduzi CCM.Pichani juu na chini ni gari iliyopelekea kifo cha Shabiki huyo wa Yanga,Ally yanga