Fainali ya Uefa kupigwa Leo. je Mechi ya Buffon na Ronaldo? tazama hapa - EDUSPORTSTZ

Latest

Fainali ya Uefa kupigwa Leo. je Mechi ya Buffon na Ronaldo? tazama hapa





Ni fainali ya kihistoria ya Real Madrid na Juventus leo Jumamosi jijini Cardiff, Wales huku timu hizo mbili kila moja ikiwa imenyakua ubingwa wa Ligi Kuu nchini mwake msimu huu.


Real Madrid ina kibarua kigumu cha kutetea taji hilo, kutokana na Juventus iliyo katika kiwango cha juu msimu huu.


Mchezo huo wa fainali unahusisha ushindani kwa makocha, wachezaji pamoja na mfumo ndani ya uwanja.


Makocha Zinedine vs Allegri


Utamu wa fainali hiyo umekolezwa na ushindani wa kocha Zinedine Zidane ambaye ni chimbuko la klabu hiyo ya Italia. Zidane anapambana ili kuandika historia kuyakua taji hilo kwa mara ya kwanza tangua achukue mikoba kuinoa klabu hiyo Januari mwaka jana.


Pia, Kocha Massimiliano Allegri anataka kujihakikishia nafasi ya kuwa miongoni mwa makocha bora mbele ya wapinzani wao, Real Madrid.


Vita ya Ronaldo vs Buffon


Mtifuano katika fainali hiyo ipo kwa makocha pekee. Mchezaji Christiano Ronaldo anataka kudhihirisha ubora wake mbele ya kipa wa Juventus, Gianluigi Buffon.


Kipa Buffon amekuwa mahiri baada ya kuzua hatari nyingi kwenye lango lake huku akiwa ameokoa michomo 13 kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa.


Pia, Ronaldo amejikusanyia mabao matano kabla ya kukutana na kipa huyo kwenye mechi hiyo yenye ushindani.


Miongoni mwa mashuti sita aliyopiga Ronaldo, matano yalizaa mabao na moja lilitoka nje. Wachezaji hao wote wanawania tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu inayotolewa na Chama cha Soka Ulaya (Uefa) ambao ndiyo waandaaji wa mashindano hayo makubwa.


Ushindani kwenye mfumo


Kocha Allegri atashusha kikosi chake uwanjani huku akitumia mfumo wa 4-2-3. Mfumo huo amekuwa akipenda kuutumia kutokana na kuamini kwamba ndiyo umemletea mafanikio makubwa.


Zidane ataingiza timu uwanjani huku akitumia mfumo wa 3-4-3.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz