YANGA YAPATA USHINDI MNONO MKOANI GEITA YAIADHIBU BILA HURUMA BUSERESELE FC - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 2 May 2017

YANGA YAPATA USHINDI MNONO MKOANI GEITA YAIADHIBU BILA HURUMA BUSERESELE FC


Klabu ya Yanga imeibuka na Ushindi mnono ugenini  Mchezo wa kirafiki dhidi ya Buseresela Fc katika kujiandaa na Mchezo wa ligi kuu dhidi ya Prisons.

 Katika mchezo huo  Yanga imeibuka na ushindi wa goli 5 - 0 magoli hayo yakifungwa na Deus Kaseke mnamo dakika ya 45+1, Emmanuel  Martin dakika ya 48 na 73, huku la nne likipachikwa kimyani na Damian Matheo mnamo dakika ya 89, na Amissi Tambwe akikamilisha karamu hiyo ya magoli mnamo dakika 90+1, hivyo hadi dakika 90 kumalizika wenyeji Buseresele FC 0 Yanga 5.