-->

Type something and hit enter

On
Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB
Sote tunajua taabu inayopatikana ya ubebaji Begi au mabegi pale tunaposafiri kuelekea katika kituo aidha cha Mabasi, Treni au Ndege.

Adha hiyo sasa inakaribia kuondoka kabisa baada ya kufanyika mageuzi makubwa ya kiteknolojia kwa kuundwa begi la kisasa.

Travelmate ndio begi la kwanza duniani ambalo linatembea lenyewe bila kubebwa kuelekea kule ambapo muhusika wa begi anapoelekea.

Begi hilo la aina yake linalofanya safari iwe rahisi lilizinduliwa na Travemate mwaka 2016 mwezi oktoba.  
                     
Ni begi linalotumia Teknolojia ambayo hutakuwa na kazi ya kulibeba bali litakuwa linakufuata popote uendapo.

Ili liweze kufanya kazi vizuri na kumfuata mwenye begi limeunganishwa na simu kupitia GPS ili kuweza kumfatilia mmiliki wake kwa usahihi zaidi. Popote utakapoliweka utaweza kulifuatilia
kupitia GPS.Begi hilo linaweza kutembea kwa vertically (wima) na horizontally (usawa) na unaweza kuongeza mzigo juu yake na likaendelea kutembea bila ya taabu yoyote.

Pia Linaweza kupita popote bila shida yoyote. Linarekebisha mwendo wake ili liwe  nyuma yako kidogo. Kasi yake ni maili 6.75 kwa saa (sawa na 10.8km kwa saa) Begi hilo linatumia Battery ambalo unaweza kulitoa. 

Unaweza kulichaji kwa njia ya wireless au kwa njia USB. Battery yake inakaa na Chaji kwa masaa 4 likiwa linatumika. Na bila ya kutumika chaji inakaa kwa masaa 100. Unaweza kuweka LOCK kwa kutumia fingerprint.                                                                                                                                            
Begi hilo linalozalishwa Marekani linapatikana kwa rangi mbalimbali, na Bei yake linaanzia dola 399. 
Bei hilo linatarajiwa kuuzwa mwezi june mwaka huu tayari milango ya kuweka oda ipo wazi.


ANGALIA VIDEO HII..

Pakua App MPYA ya 'EDUSPORTSTZ NEWS-(Lite Version)' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment
 
Blog Meets Brand