TETESI ZA USAJILI ULAYA MAY 11 2017 - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 11 May 2017

TETESI ZA USAJILI ULAYA MAY 11 2017
BARCA INATAKA KUMSAJILI DI MARIA
Barcelona wanataka kumsajili winga wa Paris Saint-Germain Angel Di Maria majira ya joto kwa mujibu wa Mundo Deportivo .
Miamba hao wa Camp Nou wanataka mbadala wa Arda Turan, licha ya uhusiano wa Di Maria na Real Madrid, urafiki wake na Lionel Messi na Javier Mascherano unaweza kuwarahisishia Blaugrana mchakato huo.
CONTE KULAMBA DILI NONO
Bodi ya Chelsea imefikia makubaliano ya kumpa matakaba mpya ulioboreshwa Antonio Conte pamoja na fedha za usajili majira ya joto kwa mujibu wa Mirror.
The Blues wanataka kufanya hivyo kumzuia kocha huyo kujiunga na Inter ambao wapo tayari kumlipa paundi milioni 10 kwa mwaka, na wanao mpango wa kuwasajili Alexis Sanchez, Romelu Lukaku na Virgil van Dijk.


CITY KUCHUANA NA UTD KUMSAJILI SEMEDO
Chanzo cha Ureno O Jogo Kimedai kuwa Manchester City inataka kushindana na Manchester United kumsajili beki wa kulia wa Benfica, Nelson Semedo.
Pep Guardiola anapata upinzani mkubwa kutoka kwa Manchester United kumnasa mchezaji huyo kadhalika na Bayern Munich, Inter na Barcelona ambazo zote zinahitaji saini yake.

EVERTON YAWANYATIA SANDRO & KLAASSEN
Ronald Koeman amepewa nafasi kufanya mazungumzo na mshambulizi wa Malaga Sandro na kiungo wa Ajax Davy Klaassen, limeripoti Mirror.

MARSEILLE INATAKA KUMSAJILI MAHREZ
Marseille wameonesha nia ya kutaka kumsajili winga wa Leicester City, Riyad Mahrez, limeripoti gazeti la Daily Mirror.
Mwalgeria huyo anataka kuondoka King Power Stadium kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.

MAN CITY INAJIPANGA KUMSAJILI VALDES
Manchester City wanaangalia uwezekano wa kumsajili kipa wa Middlesbrough Victor Valdes, kwa mujibu wa ESPN .
Mchezaji huyo wa kimtaifa wa Hispania anatarajiwa kuondoka Riverside majira ya joto kufuatia timu hiyo kushuka daraja.
Na Pep Guardiola yupo tayari kuungana na mchezaji huyo ambaye alifanya naye kazi Barcelona baada ya Claudio Bravo na Joe Hart kushindwa kumshawishi dimbani.


ARSENAL YAMTAKA LEMAR
Arsenal imepania kumsajili winga wa Monaco Thomas Lemar uhamisho wa majira ya joto kwa mujibu wa gazeti la Daily Mirror.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa katika kiwango cha hali ya juu msimu huu na Arsene Wenger anatamani kumwongeza kwenye kikosi chake katika Emirates.
MAN UTD WANAMTAKA DIER KWA £40M


Bosi wa Manchester United boss Jose Mourinho anatarajia kuilipa Tottenham kitita cha paundi milioni 40 kwa ajili ya Eric Dier limeripoti The Mirror.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alisaini mkataba wa paundi 50,000 kwa wiki mwezi Septemba mwaka jana lakini Mashetani Wekundu wanaamini ofa yao inatoshoa kuishaiwishi Spurs.