Mambo 6 yanayosababisha Mbu kukung’ata - EDUSPORTSTZ

Latest

Mambo 6 yanayosababisha Mbu kukung’ata

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), malaria ni ugonjwa wa pili unaoua watu wengi zaidi ukikadiriwa kusababisha vifo zaidi ya 429,000 kwa mwaka 2016 duniani kote, ambapo zaidi ya 90% ya vifo hivyo vimetokea Afrika.

Licha ya vifo vingi vinavyosababishwa na malaria, lakini kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika la Kupambana na Magonjwa ya Binadamu (NIAID), mbu anayesababisha malaria huchagua mtu wa kumng’ata ambapo huwa na sababu maalum.
Hizi hapa ndizo sababu zinazopelekea mtu kung’atwa na mbu:
1: Kutoa hewa chafu
Kutoa hewa chafu (Carbondioxide) ni miongoni mwa sababu inayopelekea mbu kukung’ata ambapo kwa mujibu wa Dr. Anandasankar wa Chuo Kikuu cha California,  mbu ana uwezo wa kunusa harufu ya hewa chafu hata akiwa mbali .Watu wanaoathirika zaidi na sababu hii ni watu wanene kwa kuwa ndiyo hutoa hewa chafu inayosabishwa na kuzalishwa kwa acid inayotokana na unene.

2: Kunywa pombe 
Kwa mujibu wa Shirika la Kupambana na Magonjwa ya Binadamu (NIAID), mtu anayekunywa sana pombe yuko hatarini kupatwa na magonjwa yanayosababishwa na mbu. Hii ni kwa sababu mbu huvutika na damu ya mtu aliyelewa kutokana na virutubisho vinavyopatikana kwenye pombe

3: Kufanya mazoezi kupita kiasi
Utafiti huu unaonesha kuwa mbu jike huvutika zaidi na damu ya mtu anayefanya mazoezi kupita kiasi. Hii ni kwa sababu mtu anayefanya mazoezi kupita kiasi hutoa asidi inayoitwa Lactic ambayo hutumiwa na mbu kupata nguvu.

4: Watu wenye kundi O la damu
Watu wenye damu group O hung’atwa na mbu zaidi ukilinganisha na watu wa group A. Mbu hutegemea protini kuzalisha mayai, hivyo watu wenye damu group O huzalisha protini nyingi ukilinganisha na watu wa makundi mengine ya damu.

5: Kuvaa nguo ya rangi nyeusi
Ripoti zinaonesha kuwa watu wanaopenda kuvaa nguo za rangi nyeusi hung’atwa na mbu mara mbili zaidi ya mtu aliyevaa nguo ya rangi nyingine. Hii inasababishwa na mbu kuweza kuona rangi nyeusi kwa haraka ukilinganisha na rangi zingine.

6: Mama mjamzito
Wanawake wajawazito huathirika zaidi na magonjwa yanayosababishwa na mbu kama malaria, Zika, Dengue na homa ya manjano ukilinganisha na watu wengine. Hii ni kutokana na kundi hili la binadamu huzalisha hormon nyingi na kutoa hewa yenye carbondioxide kuliko watu wengine.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz