KIUNGO mshambuliaji wa TRA United, Ramadhan Chobwedo, ameendelea kuwa gumzo kubwa sokoni baada ya kuvutia vigogo wa soka la Tanzania, huku Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, akimwagia sifa na kumtaja kama “mali” yenye thamani kubwa.
Wakati Simba ikipewa nafasi ndogo ya kuingia rasmi kwenye mazungumzo, tayari Yanga SC na Singida Black Stars zimeanza vita ya chini kwa chini kuwania saini ya nyota huyo anayeng’ara ndani ya TRA United.
Chobwedo ameonyesha kiwango bora msimu huu na kuwa tishio kwa timu kubwa kila wanapokutana uwanjani.
Akizungumzia tetesi za Simba kuhitaji huduma ya kiungo huyo, Ahmed ameweka wazi kuwa hana mamlaka ya kuzungumzia mchezaji ambaye bado ana mkataba na klabu nyingine, akiheshimu taratibu za usajili.
Hata hivyo, hakusita kusifia uwezo wa Chobwedo, akieleza kuwa ni mchezaji mzuri, kijana na mwenye mustakabali mkubwa katika soka la ushindani.
“Nilimuangalia kwenye mchezo wetu dhidi ya TRA United na nikasema nitahitaji kumuona zaidi kwenye mechi nyingine tuliporudiana nao nimemtazama tena, kwa kweli klabu itakayofanikiwa kumpata Chobwedo itakuwa imefanya usajili bora sana,” amesema Ahmed.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani, Chobwedo kwa sasa anahusishwa zaidi na klabu mbili, Yanga , ambayo inaonyesha nia ya kuanza mazungumzo rasmi na kumpatia mkataba wa awali.
Pamoja na Singida Black Stars inayodaiwa tayari imefikia hatua ya mazungumzo na kuweka ofa mezani.
Hali hii inaashiria vita kali ya usajili, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona ni nani atakayeshinda mbio za kuinasa saini ya kiungo huyo mwenye kipaji kikubwa.
The post SIO SIMBA SIO YANGA VITA YA CHOBWEDO YAPAMBA MOTO appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/xMeKBta
via IFTTT
Post a Comment