RATIBA NZITO YAISUKUMA SIMBA KUHAMIA ARUSHA

MENEJA wa kikosi cha Simba, Patrick Rweyemamu, amesema ugumu wa ratiba ya timu yao umechangia kufanya mechi ya Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Dodoma Jiji FC kuchezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, badala ya Meja Jenerali Isamuhyo.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Simba itaanza kwa kucheza dhidi ya Tanzania Prisons Aprili 9, kabla ya kukutana na Dodoma Jiji Aprili 12 katika mchezo wa Kombe la CRDB, kisha kuhitimisha mfululizo huo kwa kuvaana na Fountain Gate Aprili 15.

Rweyemamu amesema kutokana na msongamano wa ratiba, wameona ni busara mchezo dhidi ya Dodoma Jiji kuchezwa Arusha, ili kupunguza muda wa safari kati ya Arusha na Dar es Salaam.

“Mechi dhidi ya Dodoma Jiji sisi ni wenyeji, na kikanuni tunaruhusiwa kuchagua uwanja. Tumeamua kucheza Arusha kutokana na ratiba ilivyo, kwani tunacheza Aprili 9, 12 na 15,” amesema.

Ameongeza kuwa isingekuwa rahisi kwa timu kusafiri kutoka Arusha hadi Dar es Salaam na kurejea tena Arusha ndani ya muda mfupi, jambo ambalo lingeathiri maandalizi na mapumziko ya wachezaji.

“Hii ni ratiba ngumu, hivyo tumeona hakuna haja ya kupoteza muda mwingi safarini badala yake kuwapa wachezaji nafasi ya kupumzika na kujiandaa vizuri,” amesema.

Rweyemamu amebainisha kuwa pamoja na changamoto ya uchovu wa ratiba, timu hiyo inalenga kufanya vizuri katika michezo yote mitatu.

Amesisitiza kuwa ushindi katika mechi hizo ni muhimu kwa Simba ili kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya ushindani wa mataji wanayowania msimu huu.

The post RATIBA NZITO YAISUKUMA SIMBA KUHAMIA ARUSHA appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/qiJy4b6
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post