PEDRO APANGA SILAHA ZA MAANGAMIZI DHIDI YA PAMBA

KOCHA  Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves, ameweka wazi kuwa mchezo wao ujao dhidi ya Pamba Jiji FC hautakuwa mwepesi, amesisitiza kuwa wanapaswa kujiandaa kwa umakini mkubwa ili kupata matokeo chanya.

Yanga inatarajiwa kushuka dimbani Jumatano, Aprili 8, ugenini kusaka alama tatu muhimu dhidi ya Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, Pedro amesema tangu walipowasili Mwanza, kikosi chake kimeendelea na mazoezi makali ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kabla ya pambano hilo muhimu.

Kocha huyo ameongeza kuwa licha ya kuwa na changamoto ya majeraha kwa baadhi ya wachezaji, hali inaendelea kuimarika na baadhi yao tayari wapo fiti kwa ajili ya kuivaa Pamba Jiji FC.

Amesisitiza kuwa lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanapata ushindi ili kuendelea kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao msimu huu.

“Haitakuwa mechi rahisi. Pamba Jiji FC ni timu ambayo ipo nafasi za chini, lakini hatuwezi kuibeza kwa sababu ni timu ngumu yenye wachezaji wazuri na benchi imara la ufundi,” amesema Pedro.

Kwa upande wa Yanga, ushindi katika mchezo huo utakuwa muhimu si tu kwa pointi, bali pia kuimarisha morali ya kikosi kuelekea hatua za mwisho za msimu.

The post PEDRO APANGA SILAHA ZA MAANGAMIZI DHIDI YA PAMBA appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/XqsgDB5
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post