DUBE AONYESHA NJAA MABAO, YANGA YAITANDIKA MUEMBE MAKUMBI 4-0

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Prince Dube, amerejea kwa kishindo uwanjani baada ya kupona majeraha, akionesha makali yake kwa kuiongoza timu hiyo kupata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Muembe Makumbi City katika michuano ya Kombe la Muungano.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la New Amaan Complex visiwani Zanzibar, Yanga ilianza kwa kasi na kudhibiti mchezo tangu dakika za mwanzo, jambo lililowaweka wapinzani wao katika presha kubwa.

Dube alianza kuandika bao la kwanza dakika ya 17 akimalizia pasi safi kutoka kwa Okello, kabla ya Frank Assinki kuongeza la pili dakika ya 34 kufuatia pasi ya Shekhan.

Yanga iliendelea kushambulia kwa kasi na kufunga bao la tatu dakika ya 38 kupitia Shekhan Khamis, akihitimisha kipindi cha kwanza kwa ubora mkubwa.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ile ile ambapo Dube alirudi tena kambani dakika ya 57 akifunga bao lake la pili katika mchezo huo, akimalizia pasi ya Edmund na kuhitimisha karamu ya mabao kwa Yanga.

Ushindi huo unaipa Yanga mwanzo mzuri katika michuano hiyo, huku kurejea kwa Dube kwenye kiwango bora kikiwa ni taarifa njema kwa benchi la ufundi na mashabiki wa timu hiyo kuelekea mechi zijazo.

The post DUBE AONYESHA NJAA MABAO, YANGA YAITANDIKA MUEMBE MAKUMBI 4-0 appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/IM8b2rh
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post