BARKER ATAKA SIMBA KALI ZAIDI, WASHAMBULIAJI WAPYA NJIANI

WAKATI Simba SC ikiendelea kupambana kuhakikisha inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, tayari uongozi wa klabu hiyo umeanza kufanya maandalizi ya msimu ujao kwa kuingia sokoni kusaka wachezaji wapya.

Hatua hiyo inalenga kuimarisha kikosi ili kiwe na ushindani zaidi, ambapo baadhi ya nyota tayari wamependekezwa na kocha mkuu, Steve Barker, kujiunga na timu hiyo katika dirisha lijalo la usajili.

Taarifa zinaeleza kuwa Barker ameweka wazi kuwa uteuzi wa wachezaji hao umezingatia mambo muhimu ikiwemo uwezo wao binafsi, nidhamu pamoja na kiwango walichoonesha katika klabu wanazozitumikia kwa sasa.

Imebainika kuwa kocha huyo ameainisha maeneo kadhaa yanayohitaji kuimarishwa, hususan safu ya ushambuliaji, ambapo anahitaji kusajili washambuliaji wawili watakaoongeza makali mbele ya lango.

Chanzo hicho kimeongeza kuwa Barker pia ameomba kuongezewa kiungo mkabaji mmoja pamoja na mshambuliaji mwingine wa ziada, ili kuongeza ushindani wa namba ndani ya kikosi na kuimarisha ubora wa timu kwa ujumla.

Mbali na hilo, kocha huyo ameweka wazi dhamira ya kuimarisha safu ya ulinzi kwa kusajili mabeki wawili wa pembeni watakaoongeza nguvu na ushindani katika nafasi hizo.

“Suala la kiungo mkabaji tayari tumelipatia ufumbuzi wake, lakini bado tunafanya tathmini ya kina ili kuhakikisha tunasajili wachezaji sahihi wenye ubora unaohitajika,” kilieleza chanzo hicho.

The post BARKER ATAKA SIMBA KALI ZAIDI, WASHAMBULIAJI WAPYA NJIANI appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/DlfU5Ok
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post