Walinicheka Kwa Kukosa Mtoto Kwa Miaka, Hawakujua Nilikuwa Karibu Kushuhudia Muujiza

Kwa miaka mingi nilitembea nikiwa nimeinama kichwa. Sikuwa na nguvu ya kuangalia watu machoni kwa sababu nilijua swali lingefuata. “Bado hamjapata mtoto?” Wengine hawakuishia hapo. Waliniita tasa bila huruma.

Wengine walinong’ona kuwa labda nilitoa mimba zamani na sasa ninavuna nilichopanda. Maneno yao yalikuwa kama sindano moyoni. 

Miaka ilivyozidi kusonga, ndivyo shinikizo lilivyoongezeka. Harusi tuliyofunga kwa furaha ilianza kubeba mizigo ya lawama.

Kila sherehe ya kifamilia ilikuwa jaribio jipya. Nilijikuta nikikaa kona, nikijifanya niko bize na simu ili nisiskie mazungumzo yao. 

Kila tabasamu la mwanamke mwenye mtoto lilinifanya nijisikie pungufu. Usiku nililia kimya kimya, nikimuomba Mungu aniangalie hata mara moja.

Ndoa yangu ilianza kutikisika. Si kwamba mume wangu alikuwa mbaya, lakini hata yeye alianza kubadilika. Alikaa kimya zaidi. Wakati mwingine nilihisi anaumia kama mimi, lakini hakuwa na maneno ya kunifariji.

Kulikuwa na umbali ambao haukuwepo hapo mwanzo. Hapo ndipo niliogopa zaidi. Sikuogopa kuitwa tasa tu, niliogopa kupoteza familia yangu.
Nilijaribu hospitali kadhaa. Vipimo vilifanyika. Dawa zilitumika.Soma Zaidi.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post