USAJILI WA YANGA WAZUA MJADALA, SIMBA WAONEKANA KUZIDI HATUA

MSEMAJI wa Yanga, Ali Kamwe, ameibuka na kutoa kauli nzito akimtaka Rais wa klabu hiyo, Hersi Said, kurejea moja kwa moja kwenye majukumu ya usajili kuelekea dirisha kubwa lijalo.

Kamwe amesisitiza kuwa ni muhimu kwa uongozi wa juu, akiwemo Hersi na viongozi wenzake, kushika usukani wa mchakato wa usajili badala ya kuliachia jukumu hilo benchi la ufundi pekee.

Kauli hiyo imekuja kufuatia tathmini ya usajili wa Yanga msimu huu, ambao kwa mtazamo wa wengi haujatoa matokeo yaliyotarajiwa na mashabiki wa klabu hiyo.

Ameeleza kuwa wakati Yanga ikipambana kurejesha makali yake, wapinzani wao Simba wanaonekana kufaidika zaidi na usajili walioufanya, jambo linaloanza kuleta ushindani mkali kati ya timu hizo mbili kongwe.

“Ninasimamia kauli yangu, namuomba Rais Hersi arejee kushughulikia usajili. Wachezaji tulionao ni wazuri, lakini changamoto ipo kwenye mazingira ya soka letu la Tanzania,” amesema Kamwe.

Ameongeza  kuwa Hersi ana uzoefu wa kutambua aina ya wachezaji wanaoweza kuendana na mazingira ya ndani na hivyo kuongeza nafasi ya kufanya vizuri kwa timu.

Kwa mujibu wa Kamwe, jukumu la benchi la ufundi linapaswa kubaki kwenye kutoa mapendekezo ya aina ya wachezaji wanaohitajika, huku uongozi ukihusika moja kwa moja katika kuhakikisha usajili unaofanyika unaleta tija kwa klabu.

The post USAJILI WA YANGA WAZUA MJADALA, SIMBA WAONEKANA KUZIDI HATUA appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/B5JCVze
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post