SIMBA YAMSHTUA IBENGE, ASEMA LAZIMA WAWE TAYARI KWA VITA

KUELEKEA mchezo wa Mzizima Derby, Kocha Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge, ameweka wazi kuwa anatambua ubora wa Simba huku akisisitiza kikosi chake kinapaswa kuwa tayari kwa mapambano makali.

Azam FC inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Simba katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Aprili 5. Hata hivyo, kabla ya dabi hiyo, Azam itaanza na kibarua kingine muhimu dhidi ya Singida Black Stars, mchezo ambao umepewa uzito mkubwa na benchi la ufundi.

Akizungumzia wapinzani wao, Ibenge amesema Simba ni timu kubwa inayostahili heshima kutokana na mafanikio yake ya mara kwa mara, hususan katika michuano ya kimataifa ambako imekuwa ikipeperusha vyema bendera ya Tanzania.

“Tunafahamu ubora wa Simba na umuhimu wa mchezo huu. Ni lazima tuwe tayari kwa vita, lakini kwa sasa tunaiangalia kwanza mechi ya Singida Black Stars,” amesema Ibenge.

Kocha huyo ameongeza kuwa baada ya kumalizika kwa mchezo huo, nguvu zote zitaelekezwa kwenye maandalizi ya dabi hiyo, wakilenga kuhakikisha wanaingia wakiwa katika kiwango bora ili kupambana na kupata matokeo mazuri.

Kwa ujumla, Azam inaonyesha kuchukua tahadhari kubwa kwa kila mchezo, ikijipanga hatua kwa hatua ili kujenga mazingira imara kabla ya kuivaa Simba kwenye pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu.

Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, Azam FC iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba, matokeo yanayoongeza presha na ushindani kuelekea dabi hiyo.

The post SIMBA YAMSHTUA IBENGE, ASEMA LAZIMA WAWE TAYARI KWA VITA appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/Oh8yFft
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post