SIMBA HAIYUMBISHWI NA WAPINZANI, AHMED

SIMBA SC wamesema mechi yao dhidi ya Singida Black Stars itamuliwa na nguvu na ubora wa wachezaji wao, sio mbinu za wapinzani kujaribu kuharibu mpango wao wanashuka dimbani ugenini wakilenga alama tatu muhimu.

Simba wanatarajiwa kushuka dimbani kesho kusaka alama tatu muhimu ugenini, katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Airtel Stadium uliopo Singida.

Ni mechi ambayo inaangaliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa pande zote mbili kutokana na historia ya ushindani mkali kati ya timu hizi.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema kuwa mechi za Singida Black Stars mara zote ni changamoto, si kwa sababu ya ubora wa wachezaji pekee, bali pia kutokana na fikra na mbinu walizozoea kutumia ili kujaribu kuharibu mpango wa Simba.

“Singida Black Stars pamoja na malengo yao, lengo kubwa walilolenga ni kuifunga Simba na kujaribu kuharibu mpango wetu. Safari hii itakuwa ngumu, lakini kutokana na ubora wa wachezaji wetu na morali yao ya juu, tuna imani tutapata matokeo yanayotarajiwa,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa kikosi cha Simba kimejipanga vyema, wachezaji wana ari na morali ya kupambana kwa bidii, wakilenga kusaka alama muhimu katika kila mechi. Lengo lao kuu ni kuwapa furaha mashabiki na kuhakikisha wanatimiza malengo ya timu mwishoni mwa msimu.

The post SIMBA HAIYUMBISHWI NA WAPINZANI, AHMED appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/pFENCtG
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post