Kulikuwa na vurugu kubwa katika soko moja maarufu jijini Mwanza baada ya kundi la vijana wanaojulikana kama “ma-genz” kunaswa wakijaribu kumlaghai mama mboga na kuiba kiasi cha shilingi laki moja.
Tukio hilo liligeuka fedheha kubwa baada ya vijana hao kushindwa kutoroka na kujikuta wakivuliwa nguo hadharani na wananchi wenye hasira.
Kwa mujibu wa mashuhuda, vijana hao walijifanya wateja na kuanza kuchukua bidhaa huku wakimchanganya mama mboga kwa mazungumzo mengi. Ndani ya muda mfupi, walichukua pesa kutoka kwenye droo bila yeye kugundua mara moja.
Hata hivyo, mama mboga huyo aligundua upotevu wa pesa zake na kupiga kelele. Ndipo wananchi waliokuwa karibu walipoanza kuwafuatilia vijana hao waliokuwa wakijaribu kutoroka. Hawakufika mbali kabla ya kukamatwa na umati wa watu wenye hasira kali.
Katika hali ya kushangaza, vijana hao walivuliwa nguo hadharani kama adhabu ya aibu kabla ya kukabidhiwa kwa vyombo vya dola. Tukio hilo lilivuta umati mkubwa wa watu waliokuwa wakishuhudia kila kilichokuwa kinaendelea.
Mmoja wa mashuhuda alisema, “Hii ni fundisho kwa wengine. Usimuibie mtu anayepambana kutafuta riziki yake.”
Baadhi ya wafanyabiashara katika eneo hilo walieleza kuwa wamekuwa wakikumbwa na matukio ya wizi mara kwa mara na sasa wanatafuta njia za kujilinda zaidi.SOMA ZAIDI....................

Post a Comment