LICHA ya kucheza pungufu kwa zaidi ya kipindi kimoja, Simba SC imeonyesha roho ya kishujaa baada ya kuvuna alama moja muhimu ugenini dhidi ya Petro de Luanda, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa Uwanja wa November 11, jijini Luanda, Angola.
Mchezo huo uligubikwa na presha mapema baada ya nahodha wa Simba, Shomari Kapombe, kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza, hali iliyoifanya Simba kulazimika kucheza wakiwa pungufu dhidi ya wenyeji waliokuwa wakisaka ushindi nyumbani.
Licha ya changamoto hiyo, wachezaji wa Simba walionyesha mshikamano mkubwa, wakipambana kwa nguvu kutafuta matokeo chanya huku Petro de Luanda wakijaribu kutumia faida ya idadi ya wachezaji kuimarisha ushindi wao.
Dakika ya 83, dimba la Luanda lililipuka kwa mshangao baada ya Simba kusawazisha bao na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1, matokeo yaliyochukua hisia za mashabiki wa pande zote.
Bao hilo la kusawazisha lilifungwa na Anicet Oura, aliyepokea pasi safi ndani ya eneo la hatari kabla ya kuituliza mipira wavuni, akionyesha utulivu mkubwa na kuamsha matumaini mapya kwa timu yake.
Kabla ya bao hilo, Petro de Luanda walikuwa wakilinda ushindi wao kwa nidhamu na umakini mkubwa, lakini presha ya Simba iliendelea kuongezeka kadri dakika zilivyokuwa zinayeyuka, jambo lililopelekea makosa yaliyowagharimu.
Hatimaye, juhudi za Simba zililipa, Oura akaibuka shujaa wa mchezo kwa kusawazisha matokeo na kuufanya mchezo kurejea upya katika dakika chache za mwisho, kila timu ikionyesha nia ya kusaka ushindi.
Hata hivyo, licha ya matokeo hayo, Simba tayari imeshapoteza nafasi ya kusonga mbele baada ya kushindwa kuvuka hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
The post OURA AIPA HESHIMA SIMBA, WABEBA ALMA ANGOLA appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/US68DGl
via IFTTT
Post a Comment