KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Allan Okello, amesema wameumizwa na kushindwa kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini akasisitiza kuwa bado wana malengo makubwa ya kupigania katika msimu huu.
Okello alitoa kauli hiyo kupitia ujumbe mfupi baada ya Yanga kuhitimisha safari yake katika hatua ya makundi, akieleza kuwa matokeo hayo hayaondoi dhamira ya timu kuendelea kupambana kwenye mashindano yaliyosalia.
“Inasikitisha kutofuzu kwenda hatua inayofuata, lakini bado tuna mengi ya kupigania msimu huu,” ameandika nyota huyo kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Kabylie mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Zanzibar, ushindi ambao hata hivyo haukutosha kuwavusha kwenda robo fainali.
Kauli ya kiungo huyo inaonyesha namna ambavyo wachezaji wa kikosi hicho walivyokuwa na hamasa ya kufanya vizuri kwenye anga la kimataifa licha ya kuishia hatua ya makundi.
Yanga ilimaliza kundi lake katika nafasi ya tatu, jambo lililokatisha ndoto za kusonga mbele barani Afrika.
Sasa nguvu kubwa inaelekezwa kwenye mashindano ya ndani, hususan Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho, wakiamini bado wana nafasi ya kuandika mafanikio msimu huu.
The post NDOTO ZAZIMIKA CAF, OKELLO MAPAMBANO MAPYA appeared first on Soka La Bongo.
from Soka La Bongo https://ift.tt/oVlntHv
via IFTTT
Post a Comment