MAUMIVU YA CAF, KASALI AIBEBA SIMBA KIMATAIFA

KIPA namba moja wa Simba, Mamadou Djibrila Kasali, ameendelea kung’ara barani Afrika baada ya kuingia kwenye orodha ya makipa bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika  akishindanishwa na magwiji wengine wakiwemo walinzi wa lango wa vigogo kama Al Ahly.

Mafanikio hayo yanakuja katika kipindi ambacho Simba haina tena matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, lakini kiwango cha Kasali kimeiweka klabu hiyo katika ramani chanya ya ushindani wa Afrika.

Kasali ameonyesha uimara mkubwa langoni, akifanya kazi ngumu ya kuokoa mashuti hatari na kuipa Simba uhai katika mechi zake za kimataifa, hali iliyomfanya kutambuliwa na wadau wa soka barani Afrika.

Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, hii ni wiki ya pili mfululizo kwa Kasali kuingia kwenye orodha ya makipa bora wa Afrika, jambo linaloonesha uthabiti na kiwango chake cha juu.

Ahmed amesema kutambuliwa kwa Kasali ni heshima kubwa kwa klabu na uthibitisho kuwa uongozi ulifanya maamuzi sahihi na ya haraka kumleta kipa huyo ndani ya kikosi.

Amefafanua kuwa uamuzi wa kumsajili Kasali ulifanyika baada ya Simba kukumbwa na majeraha kwa makipa wake wawili, hali iliyozua hofu kubwa miongoni mwa mashabiki wa klabu hiyo.

“Hata hivyo, Kasali ameibuka kwa kiwango cha juu, ametuliza presha na kuiweka timu salama, jambo linalotupa matumaini na kuonesha thamani yake ndani ya kikosi,” amesema Ahmed.

The post MAUMIVU YA CAF, KASALI AIBEBA SIMBA KIMATAIFA appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/S9pZYCe
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post