Je, umewahi kusema maneno kwa hasira halafu baadaye ukatamani uyameze? Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Sheila na Tom, wapenzi wa muda mrefu kutoka mjini Kisumu, ambao uhusiano wao wa miaka mitano ulivunjika ndani ya dakika kumi tu baada ya mabishano makali yaliyosababishwa na wivu na kutoelewana.
Sheila na Tom walikuwa wamepanga hata kuanzisha biashara pamoja. Walikuwa marafiki wa karibu kabla ya kuwa wapenzi. Lakini kadri muda ulivyopita, presha za maisha na kuingiliwa na marafiki zilianza kuharibu mawasiliano yao.
Siku moja Tom aliona ujumbe kwenye simu ya Sheila kutoka kwa mwanaume wa kazini. Hakusoma kwa makini, lakini alihisi wivu. Badala ya kuuliza kwa utulivu, alianza kushambulia kwa maneno.
Sheila naye hakunyamaza. Maneno makali yakarushwa pande zote mbili. Mwishowe, Tom alisema, “Ni bora kila mmoja aende kivyake.”
Ukimya wa Baada ya Mlipuko
Siku zilizofuata zilikuwa za ukimya mzito. Hakuna aliyempigia mwenzake. Lakini ndani yao, kila mmoja alihisi pengo. Sheila alijaribu kujifanya yuko sawa, lakini kila alipofika nyumbani alikumbuka vicheko vyao na mipango yao.Soma Zaidi.
Post a Comment