KUONDOLEWA CAF, CHAMA AFICHUA SIRI

KIUNGO wa Simba, Clatous Chama, ameweka wazi kilichochangia timu yake kushindwa kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuishia kuondolewa katika hatua ya makundi, ameeleza kuwa makosa madogo yameigharimu timu hiyo kufikia malengo yake.

Chama amesema moja ya changamoto kubwa ilikuwa ni kushindwa kumaliza mechi mapema kwa kutumia vyema nafasi walizozitengeneza.

Ameeleza kuwa mara nyingi walitengeneza nafasi nyingi za mabao, lakini walikosa umakini katika kuzitumia na hivyo kuwaacha wapinzani wakirejea mchezoni, ushindani wa michuano hiyo unahitaji umakini wa hali ya juu kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho.

Ameongeza kuwa kuondolewa mapema si mwisho wa safari, bali ni somo muhimu kwa kikosi kizima, wamejifunza mengi kutokana na uzoefu wa msimu huu na watautumia kama chachu ya kujipanga upya kwa ajili ya kurejea wakiwa imara zaidi msimu ujao.

“Tumeshinda mechi ya mwisho, ushindi ambao una maana kubwa sana kwetu na kwa mashabiki wetu. Umetupa morali na kujiamini zaidi tunapoelekeza nguvu zetu kwenye mashindano ya ndani  Huu ni muda wa kujipanga na kusahihisha makosa yetu ili kurejesha heshima na historia ya klabu,” amesema Chama.

Kuhusu Kariakoo Derby dhidi ya Yanga Chama amesema bado ni mapema kuzungumzia mchezo huo kwani wana ratiba ngumu kabla ya kufika hapo, kwa sasa akili zao zote ziko kwenye michezo ijayo ya ligi na kombe, wakilenga kukusanya alama muhimu.

Simba ina kibarua kizito kabla ya kukutana na Yanga Machi mosi, ikianza na michezo ya ugenini dhidi ya Tanzania Prisons, Pamba Jiji FC na Singida Black Stars, kisha kurejea nyumbani kuivaa TRA United.

Kiungo huyo amesisitiza kuwa ushindi katika michezo hiyo ni muhimu ili kujiweka katika nafasi nzuri kabla ya dabi hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki.

The post KUONDOLEWA CAF, CHAMA AFICHUA SIRI appeared first on Soka La Bongo.



from Soka La Bongo https://ift.tt/AuO9E7o
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post