Wakati mwingine changamoto za maisha si za kawaida, chukua hatua

 


Kutana na Shadrack ambaye alikuwa kijana mwenye ndoto kubwa za kimaisha. Alizaliwa na kukulia Moshi, mji wenye mandhari ya kuvutia chini ya mlima Kilimanjaro. Tangu akiwa mdogo, alitamani kuwa mfanyabiashara maarufu, mtu ambaye angeweza kujitegemea na kusaidia familia yake. Hata hivyo, safari yake ya kibiashara haikuwa rahisi.  

Mara ya kwanza alipojaribu, Shadrack alifungua duka dogo la kuuza nguo za mitumba. Alijitahidi sana, akatafuta bidhaa bora na kuwekeza akiba yake yote. Lakini baada ya miezi michache, wateja wakaanza kupungua, na hatimaye duka likafungwa. Alijifariji akisema labda hakuchagua biashara sahihi.  

Baada ya muda, alijaribu tena. Safari hii alianzisha mgahawa mdogo uliokuwa ukipika chakula cha kienyeji. Alikuwa na hamasa kubwa, akiamini watu wa Moshi na wageni wengi wangefurahia ladha ya chakula chake. Lakini mambo yalikwenda kinyume. Chakula kilikuwa kizuri, lakini kila mara alikumbwa na changamoto zisizoelezeka: vifaa kuharibika, wateja kupotea ghafla, na gharama kuongezeka bila sababu. Mgahawa nao ukafungwa.  

Shadrack hakukata tamaa. Alijaribu biashara ya kilimo cha mboga, akiamini ardhi ya Moshi yenye rutuba ingemsaidia. Alipanda nyanya na pilipili, lakini mazao yalishambuliwa na magonjwa yasiyoelezeka, na hasara ikawa kubwa. Alipojaribu tena biashara ya usafirishaji, gari lake liliharibika mara kwa mara bila sababu ya msingi.  

Kwa muda mrefu, Shadrack alihisi kama kuna mkono wa kisiri uliokuwa ukizuia mafanikio yake. Alianza kuamini labda kuna mkosi au nguvu zisizo za kawaida zinazomkwamisha. Hali hii ilimfanya awe na huzuni na kukata tamaa, akihisi ndoto zake zote zinayeyuka. Soma zaidi hapa 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post