Jana ilikuwa siku ya kipekee kwa mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize ambaye alitangazwa kushinda tuzo ya goli bora la mwaka na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) katika usiku wa tuzo nchini Morocco.
Mzize ambaye hakuweza kufika mwenyewe akiendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti hivi karibuni, alisema tuzo hiyo imemuongezea morali ya kuzidi kufanye vyema zaidi.
Mzize aliwashukuru wachezaji wenzake, makocha, viongozi na mashabiki waliomuungana mkono na kumpigia kura kwa wingi akitaja tuzo hiyo ni ya kila mmoja.
"Nawashukuru sana CAF kwa kunipa tuzo hii, naamini ni chachu kwangu, imeniongezea thamani na imeniongezea kitu kikubwa katika majukumu yangu"
"Nawashukuru pia wachezaji wenzangu kwa kuweza kupambana kupata tuzo hii, naamini hii ni tuzo yetu sote"
"Pia nawashukuru sana benchi la ufundi, viongozi na kipekee nawashukuru sana mashabiki kwa kunipigia kura na hatimaye kupata tuzo hii ya goli bora la msimu," alisema Mzize
Usikose kuzitazama mechi ya YANGA VS FAR RABAT na SIMBA VS PETRO ATLETICO LIVE kupitia Simu yako pia ukiwa na app hii utaweza kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPAAAA AU HAPAAAA au HAPAA

Post a Comment