Ni rasmi klabu ya Simba imethibitisha kumuajiri Dimitar Pantev raia wa Bulgaria kurithi mikoba iliyoachwa na Fadlu Davids
Pantev anatua Simba kwa mkataba wa miaka miwili akikabidhiwa jukumu la kusimamia malengo ya Simba msimu huu baada ya Fadlu kuondoka
Jukumu namba moja ni kuhakikisha Simba inabeba ubingwa wa ligi kuu na kufanya vyema katika michuano ya ligi ya mabingwa ambapo kazi yake ya kwanza ni kuhakikisha Simba inatinga hatua ya makundi
Pantev anatarajiwa kuanza rasmi majukumu yake siku ya Jumatatu

Post a Comment