Yanga yapania kufuzu raundi ya kwanza kibabe CAFCL

Kesho Jumamosi, Septemba 27, macho na masikio ya mashabiki wa soka Tanzania yatakuwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Young Africans SC (Yanga) itashuka dimbani kuvaana na Wiliete SC ya Angola katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Angola, Yanga ilionyesha ubabe kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0, jambo linalowapa nafasi kubwa ya kutinga raundi ya Kwanza. Kimahesabu, Yanga wanahitaji ushindi, sare, au hata kupoteza kwa tofauti isiyozidi mabao mawili ili kutinga hatua inayofuata.

Licha ya kuwa na faida ya matokeo ya awali, Wananchi wakiongozwa na kocha Romain Folz hawatabweteka. Kucheza nyumbani mbele ya mashabiki wao wenye hamasa, ni wazi Yanga itahitaji kutangaza ubabe kwa kusaka ushindi ili kuendeleza morali ya mashindano haya makubwa barani Afrika.

Iwapo Yanga itafuzu, itachuana na mshindi kati ya Silver Strikers ya Malawi dhidi ya Elgeco Plus ya Madagascar. Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 katika mkondo wa kwanza nchini Madagascar, huku marudiano yakitarajiwa kupigwa kesho nchini Malawi.

Msimu huu Yanga imeweka malengo ya angalau kufuzu hatua ya makundi na baadae kupiga hatua zaidi katika mashindano haya. Wananchi wana dakika 270 kutimiza malengo ya awali

Usikose kutazama mechi hizi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza  HAPA  au Bonyeza HApa   Au hapa pia kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post