Usiku mmoja uliokuwa umesheheni giza na ukimya mzito, mjini kulizuka taharuki kubwa baada ya wezi kuvamia na kuvunja maduka yote kwenye barabara tuliyokuwa tunafanya biashara. Kelele za kufuli zikivunjwa na milango ikipigwa ziliwafanya wenye maduka waliokuwa majumbani mwao kuamka kwa hofu, lakini hakuna aliyeweza kufika eneo la tukio kwa sababu wezi walikuwa wengi na wamejihami.
Asubuhi ilipofika, hali ya simanzi na hasira ilitanda miongoni mwa wafanyabiashara. Maduka yalikuwa yameachwa yakiwa wazi, rafu tupu, na hasara kubwa ikawa imewakumba.
Nilipofika dukani kwangu, majirani walikuwa wamejaa pale wakiwa na macho ya mshangao. Walidhani mimi pia ningekumbwa na masaibu yale yale. Lakini cha kushangaza ni kwamba lango langu lilikuwa limefungwa vilevile nilivyoacha jana usiku.
Hakuna kufuli lililovunjwa, hakuna mlango ulioguswa, na mali yangu yote ilikuwa salama kabisa. Wengine walishangaa wakajiuliza ni kwa nini wezi walipita kila duka lakini langu hawakuweza kulivunja. Wengine walidhani nilikuwa nimeajiri mlinzi wa siri, kumbe ukweli ulikuwa tofauti kabisa.
Siku chache kabla ya tukio hilo, nilikuwa nikipitia changamoto kubwa. Hali ya wizi katika eneo letu ilikuwa imeongezeka kwa kasi. Wafanyabiashara wengi walikuwa wanalalamika kwamba kila wiki kulikuwa na duka lililoporwa. Soma zaidi hapa

Post a Comment