TAARIFA RASMI KUTOKA SIMBA NI KUHUSU KOCHA MKUU WAO FADLU DAVIS


 Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ali amewataka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kupuuza tetesi zinazosambaa mitandaoni kuwa klabu hiyo imeachana na kocha wake mkuu Fadlu Davids

Ahmed amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote na lazima zipuuzwe kwa sababu zimeanzishwa kwa lengo la kuwavuruga Wanasimb katika wakati huu muhimu kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Gaborone United hapo kesho

Ahmed amesema Fadlu yuko na timu Botswana akiendelea na majukumu yake ya kukiandaa kikosi kuelekea mchezo huo

"Taarifa kuhusu Kocha Fadlu Davids kuondoka ndani ya Simba au kuachana na Simba, nataka niwaambie wanasimba kwamba taarifa hizo ni za uzushi. Mwalimu Fadlu anasimamia program ya mazoezi na vijana hapa Francistown, Botswana"

"Taarifa zinazosema Fadlu ameachana na Simba ni uzushi na ni jambo la kutaka kuvuruga kambi yetu na mipango yetu kuelekea katika mchezo uliopo mbele yetu"

"Kwetu Simba hatuna mashaka hata kidogo na mwalimu Fadlu na hatujawahi kufikiria wala kuwaza kuachana nae hasa katika nyakati hizi. Fadlu amefanya mazuri ndani ya Simba na bado tuna imani anaweza kufanya makubwa ndani ya timu yetu"

"Kupoteza mchezo wa dabi ambao wengi ndio wamekuwa wakiuchukulia kama sababu, sisi kama uongozi hatujauona kama ndio kufeli kwa mwalimu bali tunaona kuna makosa yalifanyika na mpinzani wetu akapata ushindi. Tumeshaachana na huo mchezo na sasa tunaangalia mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika tunakwenda kuichezaje siku ya Jumamosi," alisema Ahmed

Usikose kuitazama mechi hii ya GABORONE VS SIMBA pia mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza  HAPA  au Bonyeza HApa   Au hapa pia kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.

 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post