Jina langu ni Maryamu. Kwa kweli maisha yangu ya ndoa yamekuwa ya ajabu sana. Nimeolewa na mwanaume aitwaye Daniel. Huyu mwanaume ni tofauti kabisa na wanaume wengi ninaowajua. Yeye anajifanya kama mtakatifu: hajawahi kunificha simu yake, hata kama simhitaji, ananipa. Ana password za kila kitu waziwazi—kuanzia simu, M-Pesa hadi benki. Muda wote yupo huru, na wala hana hila zozote.
Lakini mimi, maisha yangu siyo safi hivyo. Kila mara nakutwa na SMS za wanaume—mara nimetongozwa, mara wananitumia ujumbe wa “baby.” Hizo ndizo zimevunja laini zangu nyingi. Lakini cha kushangaza, kwa upande wa Daniel sijawahi hata mara moja kumfuma na SMS ya ajabu au simu ya wanawake.
Mara nyingine namuangalia nikijisemea moyoni: “Huyu anajifanya malaika sana. Eeh! Nitamfuma tu siku moja, na siku hiyo tutajua nani zaidi.” Lakini jamani, wapi? Daniel amebaki kuwa mtu yule yule: mwaminifu, mpole, na kila wakati akinieleza, “Mimi nikiwa na mwanamke mmoja, ndiye huyo huyo moyoni. Wewe ndiye wa pekee kwangu, mama watoto wangu, mama yangu mzazi.” Soma zaidi hapa

Post a Comment