Jina langu ni Lina. Ninafanya biashara ya uwakala wa pesa. Nilianza na mtaji mdogo sana, nikishirikiana kwenye vikoba na michezo ya kuongezea kipato, mpaka nikafanikiwa kupata milioni moja. Baada ya hapo, nikaingia sokoni kufanya biashara yangu ya uwakala wa pesa. Hadi sasa, nimebakia na laki saba tu, na mtaji wangu unaendelea kupungua siku hadi siku.
Mume wangu David ana tabia ambazo mara nyingi sizipendi. Mwanzoni hakutaka nifanye biashara, lakini baada ya kumbembeleza, akaniruhusu. Hata hivyo, sasa ana tabia ya kutaka kutumia pesa zangu za biashara, ambazo ni za msingi.
Kwa mfano hivi karibuni, David alitoka kazini na hajafanya kazi, akarudi na elfu 10 tu kisha akanijambia:
“Sina hela ya mboga, toa hela ya mboga. Hii niliyonayo ni nauli ya kesho kwenda kazini.”
Kwa upendo namtoa, lakini moyoni naumia kwa sababu hajawahi hata mara moja kunipa hata elfu 50 kuongeza kwenye mtaji wangu. Soma zaidi hapa

Post a Comment