ALLY KAMWE ACHARUKA AWACHANA UKWELI WACHAMBUZI KUHUSU HILI


 Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amefichua kuwepo mkakati wa baadhi ya wachambuzi kutumika kupenyeza ajenda ili kuhakikisha Yanga inamtimua kocha wake Romain Folz

Licha ya mwanzo mzuri ambao Folz ameanza nao, ukiwasikiliza baadhi ya wachambuzi hasa katika vipindi vya michezo, kinachozungumzwa ni tofauti na uhalisia presha kubwa ikipelekwa kwa uongozi wa Yanga huku mashabiki wakiaminishwa timu yao haichezi vizuri kwa sababu kocha wao hana uwezo wa kimbinu

Kamwe amewataka mashabiki kutoingia katika mtego huo kwani wapinzani wao wako kazini kuhakikisha wanakosa utulivu

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Kamwe ameandika ujumbe huu;

"Kuna hizi Hoja mbili za kpuuzi sana zinaenezwa na baadhi ya wachambuzi.. Mosi, Eti Hii Yanga ya Folz siku ikikutana na mpinzani mgumu itafungwa

Pili, Eti Yanga inabebwa na uwezo wa wachezaji sio Kocha..

Hivi ni Timu gani isiyofungwa Duniani? Na tangu Lini kufungwa kukahitaji mpinzani mgumu tu? Ni mara ngapo underdogs wanashinda mechi ya mpira dhidi ya Timu kubwa?

Yanga kwa misimu ya hivi karibuni, kashinda mechi ngumu ya Derby na kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa lakini tulifungwa na Ihefu?

Yes, Mpira ni mchezo wa wazi Lakini pia ni mchezo wa FACTS pia. Yanga ingekuwa na viongozi wasiojua kitu na kuendeshwa na ajenda za kipuuzi, NABI asingeondoka Shujaa

Hoja ya pili ni hii, Eti Yanga inabebwa na wachezaji wakubwa sio Kocha? Dah .. Sasa Ulitaka Yanga ibebwe na Kobisi ndio muone ni sawa?

Hawa kina Pacome Zouzoua na wenzake wako Yanga wanakula mishahara mikubwa kwa ajili ya kumwaga jasho lao uwanjani Timu ipate matokeo mazuri

Ukimuona Pacome anapambana, Jua yuko kazini kwake.

Na kingine, ingekuwa wachezaji bora ndio wanashinda mechi, Ile PSG ya Messi, Neymar na Mbappe wangebeba sana UCL.. Msidharau Makocha kwa kiwango hiko.

Folz anashinda mechi zake, katika nyakati ngumu mno.. Ratiba ina mechi Back To Back, Mwanaume anafanya Rotatio kubwa ya Timu kulinda players na majeraha na BADO TIMU INASHINDA BILA KURUHUSU GOLI

Hii Taasisi ni kubwa na inaongozwa na watu Makini sana. Kila inapoitwa leo, Tathmini inafanywa kwa ajili ya Yanga Iwe Bora sana uwanjani.

Tunaelewa mitego yenu michafu mliyoitega kwa wachezaji wetu halafu mnajifanya kumpa presha kocha.. mfiche upuuzi wenu mlioufanya.

Ni suala la muda tu, In Shaa Allah Tutafyatua kila upuuzi wenu na Mtaumbuka kama mlivyoumbuka siku za nyuma

Tuko Vitani Wananchi.

Na vita ni kubwa kweli kweli Msimu huu.. Nawaelewa wote mliobebwa na huu mkumbo.

Niwaahidi, TUKO KAZINI TUNASHUGHULIKIA KILA KITU"

Usikose kuitazama mechi ya MBEYA CITY VS YANGA Jumanne hii LIVE kupitia Simu yako pia ukiwa na app hii utaweza kutazama mechi zote za LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA, MASHINDANO YA CAF LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza  HAPA  au Bonyeza HApa   Au hapa pia kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post