Aliyeteswa sana na vidonda vya tumbo apata suluhisho


 Jina langu ni Jane. Mwaka 2018 niligundulika nina vidonda vya tumbo. Wakati huo havikuwa vikinisumbua sana, isipokuwa nilipokula nilihisi kuungua tumboni kutokana na asidi. Mara nyingine nilipovuta pumzi, kulikuwa na harufu mbaya sana ikitoka—kama kitu kilichooza. Nilijaribu kutumia dawa mbalimbali, za hospitali na hata za mitishamba, lakini hazikunisaidia. Kwa kuwa kipindi hicho nilikuwa bado shuleni, niliamua kuvumilia maumivu bila kuelewa ukubwa wa tatizo.

Mwaka 2022 niliamua kufanya uchunguzi wa ultrasound. Majibu yalionesha sina shida kubwa. Hata hivyo, tatizo la pumzi lenye harufu mbaya lilibaki pale pale, jambo lililoninyima amani na kuendelea kunisumbua.

Mwaka 2023 hali ilizidi kuwa mbaya zaidi. Nilipata matibabu na daktari akaniambia kuwa vidonda vya tumbo vimeenea vibaya. Niliteseka sana—sikuwa na uwezo wa kula vyakula vingi nilivyovipenda kama nyanya, dagaa, wali, pilau, mboga za majani kama mchicha na tembele, wala vyakula vya kukaangwa. Nililazimika kuzingatia maji safi tu na kula kwa wakati, kwani nikichelewa kula, tumbo lilikuwa linauma sana. Hata kunywa vinywaji vya aina yoyote iliniletea maumivu makali. 

Mwaka huu bado hali ilikuwa inanisumbua. Nilipata dawa za kienyeji ambazo zilinipa unafuu kidogo. Kwa mfano, awali nilishindwa kunywa chai kabisa, lakini sasa naweza kunywa, japo bado kuna vyakula navyoepuka. Hata hivyo, tatizo kubwa lililobaki ni pumzi yenye harufu mbaya. Inanifanya nihisi kama natoka kuoza ndani. Soma zaidi hapa Soma zaidi hapa 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post