Jina langu ni Sasha, miaka michache iliyopita, kulikuwa na mwanaume aliyenitongoza, lakini nilimkataa. Baada ya hapo tulikaa muda mrefu bila kuwasiliana. Wakati huo, nilikuwa katika mahusiano mengine na hatimaye nikajikuta nimebeba mimba, hadi nikajifungua mtoto wangu.
Baada ya muda mrefu kupita, yule mwanaume wa awali alirudi tena maishani mwangu na kunitafuta. Aliniambia bado ananipenda na angependa tuwe pamoja. Nikaona ni bora nimueleze kila kitu kuhusu mimi na mtoto wangu. Cha kushangaza, hakusita, alinikubali mimi pamoja na mtoto wangu. Tukaanza mahusiano mapya kwa upendo.
Katika kipindi hicho, alinisaidia mimi na mtoto wangu kwa hali na mali. Nilihisi amani, nikaanza kumpenda kwa dhati. Mara nyingi nilikuwa nikienda kwake na kukaa siku kadhaa kabla ya kurudi kwangu. Tulikuwa vizuri kweli.Lakini baadaye, mambo yakaanza kubadilika. Alianza kuwa kimya, hakuwasiliana nami, na mara nyingi nilikuwa ndiye niliyejitahidi kumtafuta.
Hali hiyo ilinipa mashaka, na baadaye alinieleza kwamba kile tulichokuwa tunafanya hakikuwa sawa, na kwamba nisubiri afanye mipango yake kwanza kabla ya kuendelea na mahusiano yetu ya karibu. Nilijaribu kumuelewa na kukubali hali hiyo. Soma zaidi hapa

Post a Comment