Kampuni ya ubashiri wa michezo, SPORTPESA leo imesaini mkataba wa miaka mitatu kuendelea kudhamini klabu ya Yanga
Mkataba huo wenye thamani ya Tsh Bilioni 21.7, umesainiwa Serena Hotel jioni ya leo Jumatatu
Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa Mh. Tarimba Abbas alibainisha kuwa klabu ya Yanga itavuna takribani Billion 7.2 kila mwaka na kama ikibeba ubingwa wa Afrika watatoa bonasi ambayo hakuna klabu imewahi kuipata nchini
“Dhamira ya Sportpesa ilikuwa na ndoto kuingia kwenye mpira. Tuliwahi kudhamini Arsenal, Hully City, Everton, Ligi Kuu Kenya klabu kadhaa. Tulipotazama Tanzania tukabaini Yanga ni Klabu sahihi kutimiza nayo ndoto zetu. Yanga ina mashabiki wengi. Tuliwaamini sana viongozi wa Yanga kwamba tungeubadilisha mpira wa Tanzania”
"Baada ya sisi kuingia Yanga, tuliwapa nguvu ya kiuchumi. Yanga imekuwa na misuli ya kumsajili mchezaji kutoka klabu yoyote. Hii imefanya Yanga iwe na uwezo wa kumuuza mchezaji yoyote kwa sababu ina uwezo wa kumsajili mchezaji yeyote".
"Leo tumesaini mkataba mpya wa miaka mitatu. Mkataba huu ni Tshs bilion 21.7 Mkataba huu utaifanya Yanga iwe na ndoto ya kuwa Bingwa wa AFRIKA. Nje ya udhamini huu, Sportpesa Tumeweka Bonasi Kubwa kwenye mechi za kimataifa,” alisema Tarimba
Mgeni rasmi Nabu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma aliipongeza SportPesa na klabu ya Yanga kwa kuendeleza ushirikiano wao uliodumu kwa miaka nane ukiwa na tija kwa pande zote
“Niwapongeze Yanga na Sportpesa baada ya kudumu kama washirika kwa miaka nane. Mafanikio makubwa ya pande zote yametokana na ushirika huu ambao umekuwa na tija. Serikali inaendelea kutengeneza mazingira rafiki kwa wawekezaji ambayo wanayo dhamira ya kuingia kwenye mpira,” alisema
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ameipongeza SportPesa kwa kuendeleza uhusiano wake na Yanga ambao umeleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa mabingwa hao wa nchi
“Kabla ujio wa Sportpesa Yanga ilikwama. Licha ya ukubwa na ukongwe wake, Yanga ilishindwa kupata wachezaji wazuri, Yanga ilishindwa hata kusafiri bila changamoto. Lakini leo hii Yanga inagombea wachezaji wazuri na klabu kubwa Afrika."
"Mafanikio makubwa sana kutokana na udhamini mkubwa kutoka kwa Sportpesa. Tunawapongeza sana Sportpesa kwa namna ambavyo wamekuwa bega kwa bega na sisi,” alisema
Usikose kuitazama mechi za michuano ya CHAN na LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA kudownload app pia ikileta neno its harmful usiogop hii ni kwasababu bado app hatujaiweka playstore ni APK

Post a Comment