Wakati michuano ya CHAN 2024 ikiendelea kutimua vumbi katika nchi tatu jirani Tanzania, Kenya na Uganda, jina moja limeanza kutawala mijadala ya soka Afrika Mashariki: Allan Okello.
Kiungo mshambuliaji huyu wa timu ya taifa ya Uganda 'Uganda Cranes', ameibuka kuwa chachu ya mafanikio ya kikosi chake. Akiwa na kasi, ubunifu na uwezo wa kumalizia, Okello ameiongoza Uganda kushinda michezo miwili mfululizo, na hivyo kufikisha pointi 6 ambazo zimewaweka kileleni mwa Kundi C.
Katika mechi mbili zilizopita, Okello amepachika mabao mawili, mabao ambayo si tu yameipa Cranes ushindi, bali pia yameonyesha upekee wake katika kusoma mchezo na kutumia nafasi ndogo kufunga. Mashabiki na wachambuzi wametaja kiwango chake kuwa "darasa la juu", huku wengine wakimfananisha na wakali waliowahi kuichezea Uganda miaka iliyopita.
Klabu ya Simba SC imeweka wazi kuwa inatumia CHAN kama jukwaa la kusaka wachezaji wapya, jina la Okello limekuwa likizunguka mara kwa mara kwenye vyombo vya habari.
Taarifa zinadokeza kuwa mabosi wa Wekundu wa Msimbazi wanamfuatilia kwa karibu, na kiwango chake cha sasa kinaongeza uwezekano wa kumwona akivaa jezi nyekundu ya Msimbazi siku za usoni.
Usikose kuitazama mechi ya RAYON SPORT VS YANGA IJUMAA HII pia michuano ya CHAN na LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA kudownload app ikileta neno its harmful usiogop ni kwasababu bado hatujaiweka playstore ni APK

Post a Comment