Maisha ya George yalianza katika hali ya unyenyekevu sana. Alizaliwa katika kijiji kidogo cha Kakamega, katika familia maskini ya wakulima wadogo. Baba yake alikuwa akipambana na kilimo cha mihogo na mahindi, ilhali mama yake akijishughulisha na biashara ndogo ndogo ya kutengeneza sabuni ya kienyeji. George alikua akiwa na ndoto moja kubwa: kusoma hadi chuo kikuu na siku moja kupata kazi kubwa itakayobadilisha maisha ya familia yake.
Changamoto kubwa ilikuwa fedha. Ingawa alikuwa mwanafunzi hodari, akikamata nafasi za juu kila mara darasani, mara nyingi alikuwa analazimika kukaa nyumbani kwa sababu ya kukosa karo. Mara kadhaa walimu wake walichanga ili kumrudisha shuleni. Wakati wa kujiunga na chuo kikuu, hali ilikuwa ngumu zaidi. Ada ilikuwa kubwa mno na familia yake haingeweza kuimudu.
Ndipo jamii ilipoamua kuandaa harambe. Marafiki, majirani, hata walimu wake wa zamani walijitolea kidogo walichokuwa nacho. Baadhi walichangia shilingi mia tano, wengine elfu moja, na baada ya juhudi za wiki kadhaa, George alipata kiasi cha kutosha kuanza safari yake ya chuo. Soma zaidi hapa

Post a Comment