Jamaa Aandika Jina La Ex Wake Kwa Mwili Mzima Akisema Hakubali Kumpoteza Tena Kamwe

 


Wakaazi wa Mbezi Beach walishuhudia tukio lisilo la kawaida siku ya Jumatano, Julai 30, 2025, baada ya kijana mmoja kujichora jina la mpenzi wake wa zamani kwa mwili mzima akidai hawezi kuvumilia kumuona kwa mwanaume mwingine.

Kwa mujibu wa mashuhuda, kijana huyo aliyefahamika kwa jina la Edwin K., alionekana majira ya saa nne asubuhi akitembea bila shati katika mitaa ya Mbezi huku mwili wake mzima ukiwa umeandikwa jina “Sheila” kwa wino mkubwa wa kudumu. 

Maneno hayo yaliandikwa kwenye kifua, mgongo, mikono hadi mapajani. Alionekana pia ameshika ua la waridi mkononi, akisema linamwakilisha upendo wa milele ambao hauwezi kufutika.

“Tulifikiri ni maigizo ya mitandaoni,” alisema mlinzi wa duka jirani. “Lakini alipoanza kulia hadharani na kueleza alivyomuoa moyoni, tukajua hapa kuna jambo kubwa.” Soma zaidi hapa 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post