Jina langu ni Queen, nimeolewa na mwanaume ambaye tayari alikuwa na mtoto mmoja, na mimi pia nilikuwa na mtoto mmoja. Mwanzoni kabisa, aliniahidi kwamba mtoto wangu atachukuliwa kuwa wake, na mtoto wake pia atachukuliwa kuwa wangu – yaani, tungeishi wote kama familia moja yenye mshikamo na upendo. Nilifurahia sana maneno hayo kwa sababu niliona dalili za upendo na mshikamo wa familia.
Lakini baada ya kuanza kuishi pamoja, hali ikawa tofauti. Tulipoanza maisha ya ndoa, mtoto wake ndiye tulieendelea kuishi naye kila siku, huku mtoto wangu akibaki kuishi na mama yangu mzazi. Hali hiyo iliniletea maumivu makali moyoni.
Zaidi ya hayo, kulikuwa na changamoto nyingine iliyokuwa ikininyima amani. Kabla sijamuoa, mume wangu alikuwa na mwanamke mwingine ambaye familia yake yote walimpenda sana. Walipanga hata kwamba awatane naye kisheria, lakini hatimaye walitofautiana, ndipo mimi nikaingia kwenye maisha yake. Huyo mwanamke alibaki mjamzito, na alipojifungua, mama mkwe wangu alinieleza wazi kwamba mtoto alizaliwa ili upendo kati yake na mwanamke huyo usiishe – kwa sababu walikuwa wanapendana sana. Soma zaidi hapa

Post a Comment