BREAKING: ESPERANCE WATUMA OFA YA ZAIDI YA BILIONI 2.5 KUMG'OA CLEMENT MZIZE YANGA

 Download App ya Nijuze Tv kutazama mechi za ligi kuu Nbc bure, Epl, Laliga, Bundesliga, Seria A, Caf na nyinginezo pia app hii ina chanel za Azam tv na Dstv utaweza kuzitazama bure

Idownload kwa kubonyeza HAPA au HAPA


Taarifa mpya kutoka kwenye soko la usajili zinaonyesha kuwa mshambuliaji nyota wa Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania, Clement Mzize, anaendelea kuwa kivutio kikubwa kwa klabu mbalimbali barani Afrika na Kati ya Mashariki.

Hii inakuja siku moja tu baada ya Mzize kuiongoza Taifa Stars kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Madagascar, ushindi uliowawezesha kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya CHAN. Katika michuano hiyo, Mzize amekuwa moto wa kuotea mbali, akiwa kinara wa mabao kwa kufunga mabao mawili.

Awali, Yanga ilikuwa imekubaliana na klabu ya Al-Sadd SC ya Qatar kumuuza Mzize kwa kiasi cha dola 900,000. Hata hivyo, dili hilo limesuasua kutokana na kutokuwepo kwa makubaliano binafsi kati ya Mzize na Al-Sadd, hasa upande wa mshahara na maslahi mengine binafsi.

Sasa, vigogo wa Tunisia Esperance Sportive de Tunis wameingia rasmi katika mbio hizo baada ya kuwasilisha ofa ya takribani dola milioni 1 (zaidi ya Tsh bilioni 2.5) kwa Yanga. Endapo watafikia muafaka na Mzize juu ya maslahi yake binafsi, uwezekano wa mchezaji huyo kutua Tunisia ni mkubwa.

Uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa haujafunga milango ya Mzize kuondoka, mradi tu ofa iwe sahihi na iwe na manufaa kwa pande zote mbili mchezaji na klabu

Kwa kiwango anachoonyesha Mzize katika CHAN, mashabiki wa Yanga wana kila sababu ya kufurahia, lakini pia huenda wakaandaa mioyo kwa uwezekano wa kumpoteza nyota wao huyo kabla ya msimu ujao kuanza.

Kama kasi hii itaendelea, safari ya Mzize kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara hadi ligi kubwa zaidi barani Afrika au hata nje ya bara huenda ikawa ni suala la muda tu.

Usikose kuitazama mechi za michuano ya CHAN na LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA kudownload app

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post