Benchi la ufundi la Yanga limekamilika tayari kwa kazi

Benchi la ufundi la Yanga limekamilika tayari kwa kazi

Download App ya Nijuze Tv kutazama mechi za ligi kuu Nbc bure, Epl, Laliga, Bundesliga, Seria A, Caf na nyinginezo pia app hii ina chanel za Azam tv na Dstv utaweza kuzitazama bure

Idownload kwa kubonyeza HAPA au HAPA sisi kwetu michezo ni Furaha


 Kocha mkuu wa Yanga SC, Romain Folz, yuko tayari kuanza rasmi majukumu yake ya kuinoa timu hiyo ya mabingwa wa Tanzania Bara mwishoni mwa wiki hii, baada ya kukamilisha rasmi safu ya benchi lake la ufundi.

Hii ni hatua muhimu katika maandalizi ya msimu mpya wa mashindano wa 2025/26, ambapo Yanga inalenga kutetea mataji yake ya ndani na kufanya vyema zaidi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Jana, Yanga ilitangaza kikamilisho cha benchi la ufundi litakalofanya kazi bega kwa bega na Folz. Miongoni mwa majina yaliyotangazwa ni Manu Rodriguez (33), ambaye sasa atakuwa kocha msaidizi. Rodriguez anatokea Costa Rica ambako alikuwa kocha wa timu ya taifa, na tayari amewahi kushirikiana na Folz katika nafasi mbalimbali.

Katika nafasi ya kocha wa makipa, Majdi Ben Mansour Mnasria kutoka Tunisia amepewa jukumu hilo, akirithi mikoba ya Alaa Meskini aliyeondoka Februari kuelekea FAR Rabat ya Morocco.

Mnasria ni kocha mwenye uzoefu mkubwa barani Afrika, akiwa amefundisha katika klabu mbalimbali nchini Tunisia, Algeria na Afrika Kusini. Amefanya kazi na Folz hapo awali katika klabu ya Olympique Akbou (Algeria) na Lamontville Golden Arrows (Afrika Kusini).

Kwa upande wa uchambuzi wa video, Thulani Thekiso kutoka Afrika Kusini amepewa nafasi hiyo, akichukua nafasi ya Mpho Maruping aliyejiunga na CR Belouizdad ya Algeria chini ya kocha Sead Ramovic. Thekiso atakuwa na jukumu la kusaidia timu kwa uchambuzi wa kitaalamu wa mikanda ya mechi na mazoezi, jambo muhimu katika mpango wa ushindi wa Yanga.

Katika eneo la maandalizi ya viungo, Chyna Tshephang Mokaila, pia kutoka Afrika Kusini, ndiye kocha mpya wa viungo. Mokaila amewahi kufanya kazi katika klabu kadhaa barani Afrika, ikiwemo Township Rollers (Botswana), Marumo Gallants na Amazulu (Afrika Kusini), Horoya AC (Guinea), Al Ahli Tripoli (Libya), na Timu ya Taifa ya Botswana iliyofuzu Afcon 2025.

Paul Matthews, mtaalamu mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 25 katika uongozi wa kiufundi, skauti, na uchambuzi, ametangazwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi mpya wa Yanga. Matthews anachukua nafasi ya Abdihamid Moallin ambaye naye amejiunga na Sead Ramovic huko Algeria katika kikosi cha CR Belouizdad.

Kwa sasa, benchi la ufundi la Romain Folz limekamilika, likiwa na mchanganyiko wa uzoefu, taaluma na ushirikiano wa muda mrefu na kocha mkuu. Wote wako tayari kuanza safari ya kuhakikisha Yanga inaendelea kutawala soka la ndani na kuvuka hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ambayo iliwashinda msimu uliopita.

Jukumu la kwanza kwa Folz na benchi lake ni kuhakikisha Yanga inafuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika. Ni kazi yenye presha, lakini pia fursa kubwa ya kuiweka Yanga kwenye ramani ya soka la Afrika kwa kiwango cha juu zaidi. Mashabiki wa Yanga wanayo kila sababu ya kuwa na matumaini makubwa kwa msimu huu mpya.

Usikose kuitazama mechi za michuano ya CHAN na LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA kudownload app

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post