Askari mmoja wa kituo cha polisi aliibua mshangao baada ya kuamua kuvua sare hadharani na kutangaza kuacha kazi mara moja.
Tendo hilo lililotokea karibu na kituo cha polisi mchana wa saa saba liliwashangaza wengi, huku wakazi wakijitokeza kwa wingi kushuhudia. Wengi walidhani huenda askari huyo alipata mshtuko wa akili, lakini muda si mrefu ukweli wa kusikitisha ulifichuka.
Kulingana na mashuhuda wa tukio hilo, askari huyo ambaye hakutajwa jina lake kwa sababu za faragha, alikuwa akitoka doria alipopigiwa simu na jirani yake akielezwa kuwa kuna mwanaume anayeingia nyumbani kwake kila askari huyo akiwa kazini.
Aliposhtuka na kurudi ghafla nyumbani, alikumbana na hali isiyotarajiwa. Mchungaji wa kanisa maarufu mjini humo alipatikana akiwa ndani ya nyumba yake, akinywa chai na mke wake. Soma zaidi hapa

Post a Comment